CONTACT US:

CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com

Tuesday, December 22, 2015

USAJILI WA NDOA NA TALAKA

Ndugu zangu

Mambo ya ndoa na talaka nayo yana changamoto zake.  Hapa tutaangalia japo kwa kifupi kuhusiana na Jinsi ya kudai talaka na jinsi ya kufunga ndoa.

AINA ZA NDOA ●Ndoa ya mke mmoja
●Ndoa ya wake wengi

Mamlaka ya kufungisha ndoa Tanzania Bara yako mikononi mwa:
●Ndoa za serikali,
Hufungishwa na
-Wakuu wa wilaya
-Makatibu tawalawa wilaya ●Ndoa za kidini,
hufungishwa na viongozi wa dini
(maaskofu, mapadri, wachungaji, masheikh)wenye
leseni hai za kufungisha ndoa. ●Ndoa za kimila
hufungishwa mbele ya afisa
mwandikishaji (afisa tarafa) husika wa sehemu ile ndoa inapofungia.

Ndoa YEYOTE iwe ya serikali,kidini,kimila kabla ya
kufungwa lazima itangazwe kwa siku 21.

Umuhimu wakuisajili ndoa kwa msajili mkuu wa ndoa na talaka ni kama ifuatavyo:
●Kutoa utambulisho kwa wanandoa kuwa ni mke na mume, ●Cheti cha ndoa kinampa mwanandoa haki ya urithi endapo mwenzi wake atafariki, ●Cheti cha ndoa ndio uthibitisho wa ndoa kisheria, ●Cheti cha ndoa kinamwezesha mwanandoa kupata nafuu ya kodi, ●Cheti cha ndoa kinampa mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa
haki ya kurithi pasipo wosia.

TALAKA

Talaka ni ruhusa au amri ya mahakama ya kisheria
ambayo mume au mke hupewa wakati anapomwacha
mwenzi wake.

Chombo chenye mamlaka ya kutoa talaka ni mahakama tu.

Kwa waumini wa dini za kiislamu.TALAKA zitolewazo
kwa msingi wa dini ya kiislamu huwa hazivunji ndoa iliyofungwa chini ya sheria ya ndoa.
Talaka za jinsi hii kisheria zinaangaliwa kama ni nia ya kutoa
talaka.Talaka itawasilishwa mahakamani ambayo itatamka kuvunjika kwa ndoa.
TARATIBU ZA KUOMBA TALAKA ●Mwenye nia ya kuomba talaka
atapeleka malalamiko ya matatizo yake kwenye baraza la usuluhishi wa ndoa kwenye ofisi ya kamishina wa ustawi wa jamii au baraza la kata, kanisani ama BAKWATA. ●Baraza la usuluhishi la ndoa litasikiliza malalamiko na kama likishindwa kusuluhisha,hati
maalum itaandikiwa kwenda mahakamani ikieleza mgogoro huo na kutoa maoni yake kuhusu suala
husika. ●Walalamikaji/mlalamikaji atapeleka hati hiyo mahakamani kufungua shauri la kuomba ndoa
ivunjwe kisheria na staili zake kutamkwa.

Mawasiliano
Simu : 0686 484866
Email : socialworkertz@yahoo.com

1 comment:

  1. Safi sana elimu nzuri, mziweke wazi hata wengi wetu wajue vyena.

    ReplyDelete