CONTACT US:

CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com

Wednesday, December 23, 2015

SHERIA YA MIRATHI

Ndugu zangu

Vifo vingi vinatokea na kuwaacha Wajane na yatima kwenye matatizo makubwa na wasijue ni nini cha kufanya.
Mirathi Ni nini?

Mirathi ni mali aliyoacha marehemu kwa ajili ya kurithishwa warithi wake halali.

Sheria imeweka taratibu maalum zinazoongoza ukusanyaji, uangalizi, usimamizi, ugawaji na umiliki wa mali za marehemu pamoja, na kulipa madeni aliyoacha marehemu wakati wa uhai wake au gharama zitokanazo na mazishi yake.

Sheria zinazohusu urithi na wosia (mirathi) hapa Tanzania zimegawanyika katika sheria za aina tatu ambazo ni;
• Sheria ya Serikali
• Sheria ya Mila
• Sheria ya Dini ya Kiislam

SHERIA YA SERIKALI

Sheria hii inaongoza na kusimamia mgawanyo wa mali za marehemu pale ambapo itaonekana kwamba marehemu alikuwa hafuati Sheria za Kiislam wala Sheria za Kimila au kama ni waislamu hawataki sheria ya dini yao kutumika katika mirathi.

MGAWANYO WA MALI KWA KUTUMIA SHERIA HII HUWA HIVI: • Kama marehemu ameacha mjane na watoto, mjane atapata 1/3 na watoto 2/3 ya mali yote ya marehemu. • Lakini kama marehemu hakuacha watoto, basi mjane atapata ½ na ½ ya mali na nyingine inayobaki hugawanywa sawasawa kati ya wazazi, kaka, na dada za marehemu.

ANGALIZO: Mgawanyo wa mali kwa mujibu wa sheria hii hufanyika pale tu ambapo marehemu hakuacha wosia. Kama kuna wosia mali zitagawanywa kwa mujibu wa wosia.

Kwa mujibu wa sheria hii watoto wa nje ya ndoa hawana haki ya kurithi isipokuwa tu kama kuna wosia unaolekeza namna mali yake itakavyo gawanywa pindi atakapofariki.

Mawasiliano
Simu : 0686 484866
Email : socialworkertz@yahoo.com

No comments:

Post a Comment