CONTACT US:

CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com

Saturday, November 21, 2015

MTOTO JOSEPH AUWAWA KINYAMA.

Mwili wa mtoto Joseph kama ulivyokutwa kisimani.

Mtoto Joseph mwenye umri wa miaka 7 alikutwa ametupwa katika kisima cha jirani yao usiku wa kuamkia Jumatatu tar.16/11/2015, hapa Yombo vituka maarufu kama kwa Chande.

Taarifa za wazazi zinasema mtoto wao walianza kumtafuta usiku saa 2 baada ya kutoonekana nyumbani. Walitembea na kuuliza kila mahali lakuni hakukuwa na taarifa za kuonekana kwake. Baadae walitoa taarifa za katika kituo kidogo cha police yombo vituka.

Usiku huo walijaribu kuangalia katika kisima (ambacho kesho yake alionekana humo) lakini pamoja na kuingiza mti mrefu na kukoroga kwenye maji hakukuwa na dalili za kuwemo kiumbe huyo.

Kesho yake Jumatatu tar.16/10/2015. Saa 12 alfajiri, mtu mmoja aitwae Kilongola ambae ni jirani alitoa taarifa za kuona kiumbe katika kisima kilekile ambacho walikiangalia usiku.

Ilikuwa ni simanzi kubwa! Baadae police Chang'ombe waliuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi.

Taarifa zilizopatikana baada ya uchunguzi wa kitaalamu zilionyesha kabla ya kifo chake marehemu alilawitiwa kisha kunyongwa na kutupwa ktk kisima kile akiwa amekufa.

Mauaji hayo ya kikatili yanahusishwa na bw.Kilongola ambae ni jirani wa familia hiyo.

Kuna taarifa kwamba marehemu alikutwa akicheza mchezo usiofaa na binti wa Kilongola mwenye miaka 5. Tukio hilo lilishuhudiwa na mke wa Kilongola. Mke huyo hakufurahishwa na kitendo hicho cha Joseph (marehemu) kumfanyia binti yake. Alimchukua hadi kwa wazazi wake na kuwaeleza kitendo alichokuwa anafanya mtoto wao kwa bintiye.

Wazazi wa Joseph walimuadhibu mtoto wao na kumuonya asirudie tena. Waliyazungumza kama wazazi kisha wakayamaliza. Hiyo ilikuwa jumamosi tar.14/11/2015.

Bw.Kilongola aliporejea nyumbani na kuelezwa taarifa za kufanyiwa kitu kibaya mtoto wake, hazikumfurahisha na kueleza kutoridhishwa na maamuzi waliyofanya na kusema hayo ni yakwao yeye atajua cha kufanya.

Kwa sasa bwana Kilongola, mkewe na wazazi wao wanashikiliwa na jeshi la police kwa uchunguzi.

My take; Naomba jeshi la police litende haki kwa ukatili aliofanyiwa huyu mtoto. Huwezi kumuadhibu mtoto wa miaka 7 kwa kumkuta akicheza na binti wa miaka 5. Hawa wapo kwenye kipindi cha kujaribu kila kitu na hawana madhara hata wakijaribu.

Na hatuwezi kuwalaumu hawa watoto, chanzo cha haya yote ni sisi wazazi kulala chumba kimoja na kufanya mambo yetu mbele ya watoto kwa kuamini wamelala au hawajui chochote!

Bw.ametoa na Bw.ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.

N:B Mwili wa marehemu unasafirishwa mchana huu kwenda kwao Moshi kwa mazishi.

No comments:

Post a Comment