CONTACT US:

CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com

Wednesday, May 2, 2012

MISS USTAWI KUFANYIKA IJUMAA HII MAISHA CLUB

SHINDANO la kumsaka mrembo wa Chuo cha Ustawi wa Jamii 2012, linatarajiwa kurindima Ijumaa hii ndani ya Ukumbi wa New Maisha Club Masaki jijini Dar es Salaam, ambapo warembo 12 watachuana kuwania taji hilo. Akizungumza na mtandao huu mratibu wa shindano hilo, Sada Ally, alisema kuwa mchakato wa kuwaandaa washiriki hao umeshakamilika na wako fiti kimazoezi, kinachosubiliwa hadi sasa ni siku tu ya mpambano huo. “Tulianza mchakato na mazoezi tangu Aprili Mosi mwaka huu, na tunamshukuru Mungu warembo wanafanya vyema, hivyo ninawaomba mashabiki wote wahudhurie siku ya Ijumaa hii ndani ya Ukumbi wa Maisha Club ili wapate burudani kutoka kwa warembo wetu na wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva,” alisema Sada.

No comments:

Post a Comment